London,England.
Kiungo wa Chelsea Mbrazil Willian Borges da Silva Ijumaa usiku aliibuka kidedea baada ya kushindwa tuzo mbili katika sherehe zilizoandaliwa na klabu hiyo kwa ajili ya kuwatuza wachezaji waliofanya vizuri katika msimu wa 2015/2016.
Willian amekuwa mchezaji wa tatu baada ya Juan Mata na Eden Hazard kushinda tuzo zote mbili za mchezaji bora wa mwaka.Tuzo hizo ni Mchezaji bora wa mwaka wa Klabu (Chelsea Player of the Year) na Mchezaji bora wa mwaka chaguo la wachezaji (Players' Player of the Year).
Tuzo hizo zimekuja baada ya Willian kuwa na msimu mzuri zaidi Chelsea akifunga mabao 11 kati ya hayo 6 ni ya faulo (Free Kick) katika michezo 47.
WASHINDI WENGINE
Ruben Loftus-Cheek ametwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi (Young Player of the Year) baada ya kuwa na msimu mzuri akiichezea kikosi cha wakubwa cha Chelsea michezo 16 na kukifungia mabao mawili.
Tuzo ya bao bora la mwaka imekwenda kwa mchezaji bora wa msimu uliopita Eden Hazard.Bao hilo ni lile alilolifunga dhidi ya Tottenham na mchezo kuisha kwa sare ya mabao 2-2 na kuipa Leceister City ubingwa.
Katie Chapman ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake (The Ladies Player of the Year award) baada ya kuiongoza Chelsea kutwaa mataji mawili ya Super Cup ya wanawake (Women's Super League) na Kombe la FA la wanawake (Women's FA Cup)
Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Akademi (Academy Player of the Year) imekwenda kwa Fikayo Tomori.kl
0 comments:
Post a Comment