Yokohama,Japan.
Michuano ya kombe la dunia la vilabu imeanza kutimua vumbi lake leo huko Japan ambapo wenyeji Sanfrecce Hiroshima wamefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuilaza Auckland City ya Oceania kwa mabao 2-0 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa katika dimba la Yokohama International.
Mabao yaliyoipa ushindi Sanfrecce Hiroshima yamefungwa na Yusuke Minagawa na Tsukasa Shiotani.Kufuatia ushindi huo Sanfrecce Hiroshima itavaana na TP Mazembe ya Kongo katika mchezo wa robo fainali utakaopigwa siku ya jumapili huko Osaka.
0 comments:
Post a Comment