728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 24, 2015

    LECEISTER CITY KUGAWA POMBE BURE KWA MASHABIKI WAKE KATIKA MCHEZO DHIDI YA MAN CITY DESEMBA 29

    Leceister,England.

    Wamiliki wa klabu ya Leicester City kampuni ya King Power International siku ya Disemba 29 watatoa bia/pombe bure kabisa kwa mashabiki wao katika siku ambayo Leicester City itakuwa nyumbani ikiuaga mwaka 2015 kwa kuvaana na Manchester City.

    Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Leceister City kufanya tukio kama hilo kwani mara ya kwanza ilikuwa ni msimu uliopita ambapo kampuni ya King Power International ilitoa bia za kutosha kwa mashabiki kusherekea kufuatia Leceister City kunusurika kushuka daraja.

    Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Aiyawatt
    Srivaddhanaprabha amesema wanataka kuitumia siku hiyo kuwashukuru mashabiki wao ambao wamekuwa bega kwa bega na klabu hiyo ambayo msimu huu imekuwa mwiba mchungu kwa vigogo vya soka nchini England kiasi cha kuanza kubashiriwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

    Srivaddhanaprabha amesema King Power International ikishirikiana na kampuni ya kutengeneza pombe ya Singha Corporation itahakikisha mashabiki wote 30,000 watakaokuwa katika dimba la King Power wanakuwa na grasi kubwa mikononi mwao wakisherekea mafanikio hayo na kuukaribisha mwaka 2016.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LECEISTER CITY KUGAWA POMBE BURE KWA MASHABIKI WAKE KATIKA MCHEZO DHIDI YA MAN CITY DESEMBA 29 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top