Dar es salaam,Tanzania.
Magoli matatu ya Mrundi Hamis Tambwe na moja la Mzimbabwe Thabani Kamusoko yameipa Yanga ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Stand United katika mchezo mkali wa ligi kuu uliochezwa jioni ya leo uwanja wa taifa,Dar es salaam.
Tambwe ameyafunga magoli hayo dakika za 18,36 na 45 huku Kamusoko akifunga dakika ya 62 kwa kichwa akiunganisha krosi ya mlinzi Juma Abdul.
Kutoka Mwanza:Simba SC imetoka sare ya goli 1-1 na Toto Africans katika mchezo uliopunguzwa ladha na mvua kubwa iliyonyesha jijini Mwanza na kuufanya uwanja wa CCM Kirumba kujaa maji.
Goli la Simba SC limefungwa na Danny Lyanga dakika ya 22 huku Toto Africans wakisawazisha dakika ya 90+2 kupitia kwa Everist Bernard.
Matokeo mengine yako kama ifuatavyo....
0 comments:
Post a Comment