728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 23, 2015

    MAGULI KUIKACHA STAND UNITED MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

    Shinyanga

    Straika nyota wa Stand United ya Shinyanga, Elias Maguli, amedai kuwa muda wowote kuanzia sasa anaweza kuikacha klabu hiyo kama hali ya utulivu itaendelea kupotea.

    Stand United hivi sasa inakabiliwa na matatizo makubwa ya utulivu kutokana
    na viongozi wake kila wakati kuvurugana jambo ambalo limeanza kuigawa timu hiyo katika makundi tofauti.

    Maguri alisema vurugu hizo za viongozi hao zimechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kupoteza mechi zake mbili za Ligi Kuu Bara ilizocheza hivi karibuni dhidi ya Mwadui FC na Yanga.

    “Wachezaji hivi sasa wameanza kugawanyika katika makundi wakiwaunga mkono baadhi ya viongozi
    wanaowaamini.

    “Hali hiyo ndiyo hasa imechangia tushindwe kufanya vizuri katika mechi
    mbili zilizopita kwa sababu ushirikiano uliokuwepo uwanjani hivi sasa haupo
    tena kila mtu anacheza.anavyojua yeye.

    “Kama hali hii itaendelea hivi hakuna haja ya kuendelea kuumiza kichwa na timu hii inabidi tutafute njia nyingine za kufanya kwa sababu yote haya wameyataka wao,” alisema Maguli.

    Chanzo:(Saleh Jembe Blog)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAGULI KUIKACHA STAND UNITED MUDA WOWOTE KUANZIA SASA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top