LONDON,ENGLAND.
Ndoto ya Arsenal kumuona Alexis Sanchez akirejea tena dimbani mwaka huu imegonga mwamba baada ya nyota huyo kujitonesha mazoezini jeraha la misuli lililokuwa likimsumbua.
Sanchez ambaye aliumia mwezi Novemba katika mchezo ambao Arsenal ilitoka sare ya 1-1 na Norwich City alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kilichoshuka dimbani jumatatu usiku kuivaa Manchester City lakini alijitonesha kwa bahati mbaya na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu imegundulika kuwa nyota huyo bado ana tatizo katika misuli yake hivyo anahitaji muda zaidi ili aweze kupona vizuri.
Kufuatia habari hiyo mbaya Sanchez anatarajiwa kukosa michezo minne ya ligi kuu ambayo ni dhidi ya Southampton, Bournemouth,Newcastle United na Sunderland huku kukiwa na uhakika wa kuivaa Liverpool Januari 13.
0 comments:
Post a Comment