Tokyo,Japan.
RAIS wa klabu ya River Plate Rodolfo D'Onofrio amelaani vikali vitendo vya kihuni vilivyofanywa na mashabiki wa klabu hiyo kwa nyota wa FC Barcelona Lionel Messi siku ya jumapili.
Hatua hiyo ya D'Onofrio imekuja baada ya ripoti kudai kuwa Messi akiwa katika uwanja wa ndege wa Narita (Tokyo) alitukanwa na kisha kutemewa mate na mashabiki wa River Plate waliochukizwa na kitendo cha klabu yao kukung'utwa mabao 3-0 na FC Barcelona katika mchezo wa fainali wa kombe la dunia la vilabu ambao Messi alifunga bao la kwanza.
Akiongea na Fox Sports D'Onofrio amesema "Ni upumbavu.Shabikia aliyefanya kitendo kile ni mpumbavu kupindukia.Nimesoma kuwa Messi amepata wakati mgumu toka kwa mashabiki wetu.
0 comments:
Post a Comment