728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 23, 2015

    CHELSEA BHANA KWELI PESA SIYO TATIZO, YAKUBALI KUTOA £30M KWA STRAIKA MBRAZIL

    London,England.

    Chelsea imekubali kumsajili straika wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine Mbrazil Alex Teixeira kwa ada ya £30m hapo mwezi januari,hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Star la England.

    Chelsea imekuwa ikimuwinda nyota mwenye umri wa miaka 25 kwa kipindi kirefu sasa kutokana na rekodi yake nzuri ya kufumania nyavu kwani mpaka sasa Teixeira amefanikiwa kufunga magoli 22 katika michezo 15 ambayo ni idadi kubwa kuliko magoli yaliyofungwa na kikosi kizima cha Chelsea.

    Teixeira alijiunga na Shakhtar mwaka 2010 akitokea Vasco da Gama ya nyumbani kwao Brazil.Tangu wakati huo Teixeira amefanikiwa kuifungua Shakhtar jumla ya mabao 89 katika michezo 222. 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA BHANA KWELI PESA SIYO TATIZO, YAKUBALI KUTOA £30M KWA STRAIKA MBRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top