Daes salaam,Tanzania.
MENEJA wa straika wa timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mbwana Samatta, Jamali Kasongo, anaonekana ‘kuibip’ (kuichokoza) Yanga baada ya kummwagia sifa staa wa timu hiyo, Donald Ngoma.
Katika hali ambayo inaonekana kama kumtamani Ngoma, Kasongo ameliambia BINGWA kuwa straika huyo ndio mchezaji pekee wa kimataifa anayecheza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambaye ana hadhi na ubora wa kuwa ‘profeshino’.
Kisongo amedai kuwa licha ya idadi ya wachezaji wa kigeni kuongezwa kutoka wachezaji watano hadi saba msimu huu, bado wachezaji wengi wa kigeni ambao wamesajiliwa wamekuwa na uwezo sawa na wale wazawa.
Meneja huyo alisema awali Muivory Coast, Paschal Serge Wawa wa Azam ndiyo alionekana kuwa bora zaidi, lakini kwa sasa anaonekana kuanza kuchoka na kiwango chake kinaanza kuwa kama cha wazawa tu.
Kisongo alisema akiangalia kati ya wachezaji wote wa kigeni ambao wamesajiliwa wakati wa dirisha dogo na wale ambao walikuwa kwenye timu za Ligi Kuu, hakuna mwenye kiwango cha juu ambacho kinaweza kumfikia Ngoma.
(CHANZO:BINGWA)
0 comments:
Post a Comment