London,England.
Arsenal imeendeleza ubabe wake kwa Manchester City baada ya usiku wa leo jumatatu kuitandika kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliopigwa katika uwanja wa Emirates.
Mabao yaliyoipa ushindi Arsenal leo hii yamepatikana kipindi cha kwanza dakika za 33 na 45 kupitia kwa Theo Walcott na Olivier Giroud wakimalizia kazi mzuri ya kiungo Mesut Ozil.
Bao la Manchester City limefungwa na kiungo Yaya Toure kwa shuti kali dakika ya 82 akiunganisha vyema pasi ya mlinzi Bakari Sagna.
0 comments:
Post a Comment