London,England.
Mlinda mlango wa Arsenal Petr Čech amefikia rekodi ya mlinda mlango wa zamani wa Liverpool na Manchester City David James ya kucheza michezo 169 ya ligi kuu England bila ya kuruhusu goli baada ya leo kuiongoza Arsenal kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Aston Villa huko Villa Park.
Čech amefikisha idadi hiyo baada ya kushuka dimbani mara 349 huku David James yeye akifikisha idadi hiyo katika michezo 572.
Mwingine anayeikaribia idadi hiyo ni mlinda mlango wa Leceister City Mark Schwarzer aliyelinda lango lake lisiguswe na mpira mara 151 katika michezo 514.
0 comments:
Post a Comment