728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 28, 2015

    PETER CECH AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU ENGLAND

    London,England.

    Peter Cech sasa ndiye mlinda mlango aliyecheza michezo mingi zaidi ya ligi kuu England bila ya kuruhusu goli hata moja baada ya leo usiku kuiongoza Arsenal kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Bournemouth katika mchezo uliopigwa katika dimba la Emirates.

    Baada ya kufanikiwa kuizuia michomo ya washambuliaji wa Bournemouth isiguse nyavu zake Cech,33 amefikisha cleen sheet 170 baada ya kucheza mchezo 352 na kufanikiwa kuivunja rekodi ya kucheza michezo mingi ya ligi kuu bila kufungwa (clean sheet) iliyokuwa ikishikiliwa na mlinda mlango wa zamani wa Liverpool, Aston Villa, West Ham,Manchester City and Portsmouth Muingereza David James ya cleen sheet 169 katika michezo 572.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PETER CECH AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top