Sunderland,England.
Ikiwa ugenini Liverpool imeumaliza mwaka 2015 kwa staili ya aina yake baada ya jumatano usiku kuilaza Sunderland kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliopigwa katika dimba la Stadium of Light,Sunderland.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Mbelgiji Christian Benteke dakika ya 46 akimalizia pasi nzuri ya Adam Lallana na kuipa Liverpool ushindi wa pili mfululizo baada ya wikendi iliyopita kuilaza Leceister City kwa bao 1-0.
Kufuatia ushindi huo Liverpool imechupa mpaka nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 30 sawa na mahasimu wao Manchester United lakini ikizidiwa kwa tofauti ya magoli.
0 comments:
Post a Comment