Leceister,England.
Leceister City imerejea kileleni mwa ligi kuu nchini England baada ya usiku wa leo kuibamiza Chelsea kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la King Power,Leceister.
Leicester City imepata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji wake hatariJamie Vardy aliyefunga dakika ya 34 akiunganisha krosi safi ya Riyad Mahrez.
Bao la pili la Leicester City limefungwa dakika ya 48 na Riyad Mahrez baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa kulia wa Chelsea Cesar Azipilicueta aliyekuwa akicheza mchezo wake wa 100 na kumtungua mlinda mlango Thibaut Courtois.
Bao la kufutia machozi la Chelsea limefungwa dakika ya 77 na mshambuliaji Mfaransa Loic Remy aliyeunganisha krosi ya Pedro Rodriguez.
0 comments:
Post a Comment