LYON,UFARANSA
Klabu ya Olympique Lyon inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa [Ligue 1] imemteua Bruno Genesio kuwa kocha wake wa muda baada ya kumfuta kazi Hubert Fournier.
Genesio,nyota wa zamani wa Lyon ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa msaidizi wa Fournier atashikiria jukumu hilo mpaka mwisho wa msimu.
Genesio ataianza kazi yake hiyo mpya siku ya jumatatu kwa kusimamia mazoezi kabla ya Januari 3 kushuka dimbani kuvaana na Limoges katika mchezo wa kombe la chama cha soka cha Ufaransa [France Cup].
SABABU ZA KUFUTWA KAZI KWA FOURNIER
Lyon imeamua kumfuta kazi Hubert Fournier baada ya kujikuta ikishindwa kufurukuta katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya huku ikimaliza hatua ya makundi ikiwa mkiani mwa kundi H na kukosa hata nafasi ya kushiriki Europa Ligi.
Aidha sababu nyingine ni kuwa Lyon imeendelea kupata matokeo mabovu katika michezo yake ya Ligue 1 kwani mpaka sasa inashika nafasi ya tisa ikiwa nyuma ya vinara PSG kwa pointi 25.
0 comments:
Post a Comment