Southampton,England.
Kocha Mkuu wa klabu ya Southampton Mholanzi Ronald Koeman amevionya vilabu vyote pinzani vya England kwamba haitawezekana kusajili mchezaji yoyote yule toka katika klabu yake hapo mwezi januari akiwemo Mkenya Victor Wanyama anayewindwa vikali na vilabu vya Arsenal na Tottenham.
Koeman amesema klabu yoyote ile itakayoonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji wake yoyote yule itakuwa inapoteza tu wakati kwani hakuna mchezaji yoyote atakayehama Southampton ifikapo mwezi Januari.
Akiongea na Sky Sports Koeman amesema "Acha waandae dau lolote lile wanalotaka kuandaa lakini ifikapo Januari hakuna mchezaji atakayeondoka.Wanaongelea wachezaji wetu kwa sababu Southampton tuna wachezaji wazuri.
Wanatumia ligi ya mabingwa kuwashawishi lakini wanapaswa kukumbuka kuwa tuna aina yetu ya kufanya biashara,hakuna atakayeondoka Januari.
Kauli hiyo ya Koeman imekuja wakati ambapo wachezaji wake wawili nyota Victor Wanyama na Sadio Mane wameripotiwa kutakiwa kwa udi na uvumba na vilabu vikubwa vya ndani na nje ya England.Vilabu hivyo ni Arsenal,Tottenham,Manchester United na Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment