Barcelona,Hispania.
HATARI SANA hii ndiyo kauli rahisi unayoweza kuitumia kuelezea tukio lililofanywa na klabu ya FC Barcelona siku ya jana jumatatu baada ya kusajili mchezaji na kisha kumtema masaa saba baadae.
Habari iko hivi.FC Barcelona siku ya jana jumatatu ilimsajili kiungo Sergi Guardiola,24 kwa ajili ya kuichezea klabu yake ya pili ya FC Barcelona B inayoshiriki ligi ya daraja la pili (Segunda).
Lakini kama ilivyo kawaida kwa mashabiki wa soka kuanza kuchimbua mambo ili kujua mengi kuhusu wachezaji wao wapya,balaa likafumuka baada ya mashabiki kuingia katika ukurasa wa twitter wa Guardiola na kukutana na ujumbe (post) iliyokuwa ikiitukana FC Barcelona pamoja na nahodha wake Lionel Messi huku akionyesha kuiunga mkono klabu pinzani ya Real Madrid.
Baada ya habari hiyo kuwafikia vigogo wa FC Barcelona hakukuwa na kitu cha kusubiri bali kumtema nyota huyo aliyewahi kukipiga na klabu ya Alcorcon.
0 comments:
Post a Comment