London,England.
Majaaliwa ya mashabiki wa Arsenal kumuona kiungo Mkenya Victor Wanyama akijiunga na klabu yao mwezi Januari huenda yakakwama baada ya taarifa kudai kuwa kocha Arsene Wenger anafikiria kufuta mpango huo na badala yake atamsajili kiungo wa FC Basel Mmisri Mohamed El-Nenny,23.
Taarifa kutoka gazeti la Daily Mirror zinasema Arsenal iko tayari kumsajili kiungo huyo wa ulinzi mwenye thamani ya £5m baada ya kumfuatilia kwa kipindi kirefu sasa.
Sababu inayodaiwa kuifanya Arsenal ifikirie kuachana na Wanyama ni kuwa inaona kuwa kiungo huyo ni ghari sana kwani klabu yake ya Southampton imesema haitamuuza kwa dau la chini ya £25 millioni.
MAFANIKIO
Mohamed El-Nenny amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya ligi ya Uswisi akiwa na FC Basel aliyojiunga nayo Januari 2013.
0 comments:
Post a Comment