Barcelona,Hispania.
Shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya (UEFA) kupitia mtandao wake wa Uefa.com leo jumanne limetoa majina kumi na moja (11) ya wachezaji waliofanya vizuri zaidi katika hatua ya makundi kwa mwaka 2014/2015 lakini kukiwa hakuna jina hata moja la nyota toka FC Barcelona kama Messi,Suarez naNeymar licha ya klabu hiyo kuwa ya kwanza kutinga hatua ya 16 bora.
Katika orodha hiyo vilabu vya Bayern Munich na Paris Saint-Germain vimefanikiwa kutamba baada ya kila kimoja kutoa nyota wawili wawili.Kutoka Bayern Munich nyota waliotajwa ni Thomas Muller na David Alaba huku kutoka Paris Saint-Germain ni Kevin
Trapp na Thiago Silva.
Nyota waliokosekana katika orodha hiyo licha ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi ni Luis Suarez,Lionel Messi,Neymar Jr (FC Barcelona) Robert
Lewandowsk (Bayer Munich)
Artem Dzyuba (Zenit) na
Olivier Giroud (Arsenal)
KIKOSI KAMILI KIKO KAMA IFUATAVYO....
GK: Kevin Trapp (PSG)
DF: Andrea Barzagli (Juventus)
DF: Thiago Silva (PSG)
DF: Diego GodÃn (Atletico)
DF: David Alaba (Bayern)
MF: Sven Kums (Gent)
MF: Willian (Chelsea)
MF: Raheem Sterling (Manchester City)
FW: Thomas Muller (Bayern)
FW: Hulk (Zenit)
FW: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
0 comments:
Post a Comment