728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, December 17, 2015

    COPPA ITALIA:JUVENTUS,NAPOLI ZAFUZU ROBO FAINALI,ROMA,FIORENTINA ZATUPWA NJE NA VIBONDE

    Turin,Italia.

    Klabu ya Juventus imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Coppa Italia baada ya kuwatandika mahasimu wao Torino kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliopigwa katika dimba la Juventus Arena.

    Magoli yaliyoipa ushindi huo mnono Juventus yamepatikana dakika za 28 51 kupitia kwa Simone Zaza na dakika ya 73 kupitia kwa Paulo Dybala huku lile la mwisho likifungwa kwa faulo na kiungo Paul Pogba dakika ya 82.

    Katika mchezo mwingine wa Coppa Italia AS Roma imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha penati 4-2 toka kwa Spezia iliyoko Seria B baada ya kucheza dakika 120 bila ya kufungana.

    Kama ilivyo kwa AS Roma, Fiorentina inayoshika nafasi ya pili katika ligi ya Seria A imefunga na Carpi imefungwa na Capri iliyoko mkiani kwa goli 1-0 lililofungwa na Antonio Gaudio.

    Kwingineko magoli matatu yaliyofungwa na Omar El Kaddouri, Dries Mertens na Jose Callejon yameipa Napoli ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Hellas Verona.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPPA ITALIA:JUVENTUS,NAPOLI ZAFUZU ROBO FAINALI,ROMA,FIORENTINA ZATUPWA NJE NA VIBONDE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top