Birmingham, England.
Arsenal imekalia kiti cha uongozi wa ligi kuu England baada ya jioni ya leo kuifunga Aston Villa kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Villa Park huku Birmingham.
Magoli ya Arsenal yamepatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa Oliver Giroud aliyefunga dakika ya 8 kwa mkwaju wa penati uliotolewa baada ya Theo Walcott kuangusha katika eneo la hatari na Allan Hutton.
Goli la pili limefungwa na Aaron Ramsey dakika ya 38 akimalizia pasi ya Mesut Ozil na kumfunga kirahisi kipa wa Aston Villa Brad Guzan.
Kufuatia ushindi huo Arsenal imefanikiwa kuongoza ligi baada ya kufikisha pointi 33 ikiishuka Manchester City yenye pointi 32 huku Aston Villa ikiendelea kusota mkiani baada ya kujikusanyia pointi 6 katika michezo 16.
0 comments:
Post a Comment