Mashabiki wa Zamalek
CAIRO,MISRI.
Miamba ya soka la Misri klabu ya Zamalek huenda ikakumbana na adhabu kali ya kushushwa mpaka daraja la nne baada ya jana jumatatu kutangaza kujitoa katika ligi kuu ya nchi hiyo kufuatia kukasilishwa na maamuzi mabovu ya mwamuzi.
Zamalek ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Misri jana jumatatu walitoa taarifa kwenye mtandao wao kuwa wameamua kutoendelea na ligi hiyo ikiwa ni ishara ya kupinga uonevu waliofanyiwa siku ya jumapili.
Uamuzi huo wa Zamalek umekuja baada ya siku ya jumapili kupokea kipigo cha magoli 3-2 toka kwa El-Gaish.
Katika mchezo huo Zamalek wanadai mwamuzi Mahmoud Al Banna ambaye kabla ya mchezo huo walimkataa na kukitaka chama cha soka cha Misri kumbadilisha aliamua kwa makusudi kuipendelea El-Gaish kwa kuipa penati mbili za ajabu ajabu pamoja na kumtoa mlinzi wake Ali
Gabr kwa kadi nyekundi ya utata.
Kufuatia uamuzi huo wa kujiondoa kushiriki ligi kuu Zamalek huenda ikashushwa mpaka daraja la nne hiyo ni kwa mujibu wa sheria zinazoongoza soka la nchi ya Misri.
Wachezaji wa Zamalek wakishangilia goli
0 comments:
Post a Comment