728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, December 26, 2015

    MAN UNITED HOI TENA EPL,YANYUKWA 2-0 NA STOKE CITY BRITTANIA

    STOKE,ENGLAND.

    Magoli mawili yaliyofungwa na washambuliaji Bojan Krkic na Marko Arnautovic dakika za 19 na 26 yameipa Stoke City ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo mkali wa mapema wa ligi kuu England uliopigwa mchana wa leo katika dimba la Brittania.

    Stoke City iliandika goli la kuongoza kufuatia makosa yaliyofanywa na winga Memphis Depay ambaye mpira wake wa kichwa aliotaka kumrudishia mlinda mlango David De Gea kunaswa na Glen Johnson ambaye alimpasia Bojan na kufunga kirahisi.

    Goli la pili la Stoke City limepatikana baada ya Arnautovic kuuwahi mpira wa adhabu ukiopigwa na Bojan na kufunga kwa kuti kali la mbali ambalo lilimuacha David De Gea akichupa bila mafanikio.

    Kufuatia kipigo hicho Manchestet United imeshuka mpaka nafasi ya 6 baada ya kubaki na pointi zake 29 baada ya kushuka dimbani mara 18. Mchezo ujao Manchester United itakuwa nyumbani kuvaana na Chelsea.

    THE TEAMS
    Stoke: Butland, Johnson, Shawcross,Wollscheid, Pieters, Whelan (van Ginkel 46),Cameron (Adam 75), Shaqiri (Diouf 65),
    Afellay, Arnautovic, Bojan.
    Subs not used: Haugaard, Joselu, Wilson,Walters.


    United: De Gea, Young, Smalling, Jones, Blind,
    Carrick, Herrera (Pereira 82), Mata, Fellaini,Memphis (Rooney 46), Martial.
    Subs not used: Romero, Borthwick-Jackson,
    McNair, Varela, Schneiderlin.
    Booked: Young, Pereira

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN UNITED HOI TENA EPL,YANYUKWA 2-0 NA STOKE CITY BRITTANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top