Lagos,Nigeria.
Waziri wa vijana na michezo wa Nigeria Solomon
Dalung amekiagiza chama cha soka cha nchi hiyo Nigeria Football
Federation (NFF) kuacha mara moja tabia yake ya kuleta ujanja ujanja katika mauzo ya wachezaji wa kikosi cha Nigeria U-23 nje ya nchi bila ya kufuata taratibu stahiki.
Kwa mujibu wa msemaji wa waziri huyo aitwaye Nneka
Anibeze,amesema waziri Dalung alitoa agizo hilo jana jumanne huko Abuja baada ya kupata taarifa kuwa NFF imekuwa ikiratibu uuzwaji wa wachezaji vijana bila kufuata taratibu
Waziri Dalung ameonya kuwa vibali vya uhamisho wa kimataifa (ITC) havipaswi kutolewa kabla ya kukidhi matakwa ya mchezaji husika.
"Nimegundua kwamba wachezaji vijana ambao ndiyo chanzo cha fahari ya taifa letu wamekuwa wakidanganywa na kulazimishwa kusaini mikataba pasipo kujua hata asilimia moja ya kile kilichomo katika mikataba hiyo.
"Nimeiagiza NFF ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa leseni/vibali vya hawa wachezaji kuachana mara moja na tabia hiyo ambayo huwafanya wachezaji kuwa watumwa na badala yake wafuate taratibu zote stahiki katika mikataba"
“Hakuna sababu ya kukaa chini na kutazama wachezaji wetu wakiuzwa kiujanja ujanja na jasho lao likishibisha matumbo ya mawakala na viongozi wa wachache wasiyo waaminifu"Alimaliza Dulang
0 comments:
Post a Comment