London,England.
Arsenal imekaa kileleni mwa ligi kuu England kwa muda baada ya kuifunga Bournemouth kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa usiku wa leo katika dimba la Emirates.
Magoli yaliyoipa ushindi Arsenal yamepatikana dakika za 27 na 63 kupitia kwa mlinzi Gabriel Paulista aliyefunga kwa kichwa akiunganisha kona ya kiungo Mesut Ozil kisha Ozil kufunga akimalizia pasi ya kisigino toka kwa Olivier Giroud.
Kufuatia ushindi huo Arsenal imefanikiwa kuongoza ligi baada ya kufikisha pointi 39 ikiishuka mpaka nafasi ya pili Leceister City yenye pointi 38 ambayo kesho jumanne itakuwa nyumbani King Power kuvaana na Manchester City.
Katika mchezo mwingine Manchester United na Chelsea zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo ulipigwa katika dimba la Old Trafford,Manchester.
Matokeo mengine
Westham 2-0 Southampton
Watford 1-2 Tottenham
Everton 3-4 Stoke City
West Brom 1-0 Aston Villa
Crystal Palace 0-Swansea City
0 comments:
Post a Comment