OVIEDO,HISPANIA.
Mshambuliaji wa zamani wa Swansea City Miguel Perez Cuesta "Michu" amejiunga na klabu ya Langreo inayoshiriki ligi daraja la nne nchini Hispania maarufu kama Tercera.
Michu,29 amejiunga na klabu hiyo inayofundishwa na kaka yake Hernan Perez baada ya kufanya nayo mazoezi tangu mwezi Novemba alipotemwa na Swansea City kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Michu anayetarajiwa kuanza kuichezea Langreo Januari 4 wakati dirisha la usajili litakapokuwa limefunguliwa aliichezea Swansea City michezo 67 na kuifungia magoli 28 huku baadhi ya magoli hayo akiyafunga dhidi ya vilabu vya Liverpool,Arsenal na Manchester United.
0 comments:
Post a Comment