728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, December 19, 2015

    RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA:SIMBA,YANGA,AZAM ZOTE DIMBANI LEO

    Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kutimua tena vumbi lake leo jumamosi na kesho jumapili kwa timu zote 16 kushuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu ili kujiweka sawa katika msimamo.

    Vinara Yanga leo watakuwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wakiikaribisha Stand United huku Azam FC wao wakiwa wageni wa Majimaji huko Songea na pale CCM Kirumba Toto Africans watakuwa wakitoana jasho na Simba SC. 

    Ratiba kamili iko kama ifuatavyo na michezo yote itaanza saa 10:00 jioni.

    Leo; Desemba 19, 2015
    Yanga SC vs Stand United
    Mwadui FC vs Ndanda FC
    Kagera Sugar vs African Sports
    Prisons vs Mtibwa Sugar
    Toto Africans vs Simba SC
    Majimaji vs Azam FC

    Desemba 20, 2015
    JKT Ruvu vs Coastal Union
    Mbeya City vs Mgambo JKT

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA:SIMBA,YANGA,AZAM ZOTE DIMBANI LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top