Dubai.
Lionel Messi na FC Barcelona jana jumapili waliibuka vifua mbele baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na klabu bora ya mwaka katika tuzo za Globe Soccer Awards 2015 huko Dubai.
Messi aliibuka mshindi baada ya kumshinda mshindi wa mwaka jana wa tuzo hiyo Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Gianluigi Buffon wa Juventus.
Mgawanyo wa tuzo ulikuwa kama ifuatavyo....
Klabu bora ya mwaka:FC Barcelona
Rais bora wa klabu:Josep Maria Bartomeu (FC Barcelona)
Tuzo ya kocha bora wa mwaka imeenda kwa kocha wa timu ya taifa Ubelgiji Marc Wilmots akiwabwaga Luis
Enrique wa FC Barcelona na Antonio Conte wa Juventus.
Tuzo ya heshima:Andrea Pirlo na Frank Lampard
Wakala bora wa mwaka :Jorge Mendes
0 comments:
Post a Comment