728x90 AdSpace

Saturday, December 19, 2015

WAYNE ROONEY KUWEKA REKODI MPYA LEO


Manchester, England.

Wayne Rooney leo jioni anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa10 wa Manchester United kuwahi kuichezea klabu hiyo jumla ya michezo 500 katika michuano yote.

Rooney,30 aliyejiunga na Manchester United mwaka 2004 akitokea Everton anatarajiwa kuweka rekodi hiyo wakati atakapowaongoza mabingwa hao wa zamani wa EPL kuvaana na Norwich City katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.

Rooney aliyekuwa nje ya dimba kwa majuma matatu akiuguza jeraha la kifundo cha mguu (Enka) alilolipata katika mchezo ambao Manchester United ililazimishwa sare ya goli 1-1 na Leceister City anarejea huku timu ikiwa haijashinda mchezo wowote tangu alipoumia.

Mbali ya Rooney wachezaji wengine watakaorejea dimbani leo baada ya kupona majeraha yao ni Chris Smalling na Ander Herrera huku Ashley Young yeye akitarajiwa kuwa fiti wiki ijayo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: WAYNE ROONEY KUWEKA REKODI MPYA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown