Antalya,Uturuki.
Klabu ya Antalyaspor kupitia kwa Rais wake Gültekin Gencer imemteua nahodha na mshambuliaji wake Mcameroon Samwel Eto'o kuwa kocha wake wa muda baada ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Simsek.
Eto'o aliyetua klabuni hapo mwezi juni mwaka huu akitokea Sampdoria ya Italia atakuwa akisaidiana na kocha wa vijana cha klabu hiyo Mehmet Ugurlu katika kipindi ambacho Antalyaspor inasaka kocha wa kudumu.
0 comments:
Post a Comment