Yanga SC imeendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara baada ya leo jioni kuilaza Mbeya City kwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Yanga ulianza kujihakikishia ushindi dakika ya 36 baada ya Hamis Tambwe kufunga kwa shuti la karibu akiunganisha krosi ya Simon Msuva.
Goli la pili la Yanga limefungwa na Hamis Tambwe dakika ya 64 na kuwa goli lake la 10 katika ligi kuu.Goli la tatu la Yanga limefungwa dakika ya 66 na kiungo Thamani Kamusoko.
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko Kambarage Shinyanga Simba SC imetoka sare nyingine kanda ya ziwa baada ya leo tena kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Mwadui FC.
Goli la Mwadui FC limefungwa dakika ya 76 kwa kisigino na kiungo Nizar Khalfan huku lile la Simba SC likifungwa dakika ya 85 na Brian Majegwa akimalizia kazi nzuri ya Mwinyi Kazimoto.
0 comments:
Post a Comment