728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 21, 2015

    GOR MAHIA NJIA PANDA MAPINDUZI CUP

    Nairobi,Kenya.

    MTU KATI!!Klabu ya Gor Mahia imepanga kuitisha mkutano wa dharura mapema wiki hii ili kujadili ishiriki michuano ipi kufuatia kuwa na mialiko mitatu itakayoanza kutimua vumbi lake Januari,2016.

    Michuano ya Kwanza:Gor Mahia "K’Ogalo" imethibitisha kupokea mwaliko toka St.
    George FC kwa ajili ya kushiriki michuano ya kumbukumbu ya kutimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo tajiri ya Ethiopia.Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi lake Januari 10 mpaka 15.

    Michuano ya Pili:Ni Mapinduzi Cup itakayoanza Januari 2 na kufikia tamati Januari 13 huko Zanzibar ambayo hushirikisha timu nane.

    Michuano ya Tatu:Ni Fidel Odinga Memorial Cup itakayoanza Januari 9 mpaka 30.Michuano ya Fidel Odinga Memorial Cup ni ya kuazimisha kumbukumbu ya kifo cha Fidel Odinga [Raila Amollo Odinga mtoto wa waziri Mkuu wa zamani wa Kenya] aliyekuwa shabiki mkubwa wa Gor Mahia ambaye kifo chake bado ni kitendawili mpaka leo hii.

    Kupitia mkutano huo Gor Mahia itaamua ishiriki michuano ipi na iache ipi.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: GOR MAHIA NJIA PANDA MAPINDUZI CUP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top