ARMENIA
Kiungo wa Borussia Dortmund Henrikh
Mkhitaryan ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Armenia kwa mara ya tano mfululizo huku jumla ikiwa ni mara yake ya sita.
Mkhitaryan,ambaye amefunga magoli sita mpaka sasa na kupika mengine 11 katika michezo 16 ya ligi ya Bundesliga alitwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2009.
Mshindi wa tuzo hiyo hupatikana kwa kupigiwa kura na wanachama wa chama cha soka cha Armenia,Makocha,Manahodha wa vilabu na Marais wa vilabu vya ligi kuu ya Armenia,Waandishi wa habari na Wawakilishi wa vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment