LIVERPOOL,ENGLAND.
Mlinzi wa Liverpool Martin Skrtel atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata jeraha katika misuli yake katika mchezo wa ligi kuu ambapo miamba hiyo ya Anfield ilikubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa Watford wikendi iliyopita.
Skrtel,31 anaiacha Liverpool ikiwa katika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi kuu huku ikiwa imevuna pointi moja pekee katika michezo mitatu iliyopita ya hivi karibuni.
Mbali ya Skrtel Liverpool pia inatarajiwa kuwa bila ya mlinzi wake Dejan Lovren ambaye pia nae ni majeruhi hivyo tumaini pekee kwa klabu hiyo ambayo wikendi hii itavaana na vinara Leceister City litakuwa kwa walinzi wake Kolo Toure na Mamadou Sakho.Skertel ataukosa pia mchezo dhidi ya Arsenal Januari 13.
0 comments:
Post a Comment