728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 28, 2015

    MBWANA SAMATTA AILETEA NEEMA NYINGINE SIMBA SC

    Dar es salaam,Tanzania.

    Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC wanatarajia kupata asilimia 20 ya pesa za mauzo ya mshambuliaji wake wa zamani Mbwana Samatta ambaye mwezi januari mwakani atajiunga na KRC
    Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Congo.

    Kwa mujibu wa makamu wa Rais wa klabu hiyo Godfrey Nyange Kabulu,Simba SC itapata mgao huo kutokana makubaliano ya kimaandishi iliyoyafikia na TP Mazembe mwaka 2011 wakati ikimuuza nyota.

    Habari za ndani zilizoifikia Soka Extra zinasema kwamba Samatta atajiunga na KRC Genk kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 2.5 ambayo itamuwezesha kusaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuwachezea mabingwa hao wa zamani wa Ubelgiji.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MBWANA SAMATTA AILETEA NEEMA NYINGINE SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top