Tanga,Tanzania.
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo mmoja pekee,ambapo mabingwa watetezi,Yanga SC watashuka katika dimba la Mkwakwani mkoani Tanga kuvaana na wenyeji wao African Sports .
Mchezo wa leo ni wa pili kwa Yanga kucheza mkoani Tanga baada ya wikendi iliyopita kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union.
Ikiwa Yanga itapata ushindi dhidi ya African Sports leo itakuwa imefikisha pointi 27 na kukaa kileleni mwa ligi kuu ikiishusha Azam FC yenye pointi 26.
Ligi hiyo itaendelea tena Desemba 19,2015 kwa michezo sita kupigwa
Ndanda FC vs JKT Ruvu
Yanga SC vs Mbeya City
Majimaji vs Prisons
Mwadui FC vs Simba SC
Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT
Coastal Union vs Stand United
0 comments:
Post a Comment