728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, December 14, 2015

    MAHREZ ACHEKELEA KUFANANISHWA NA MESSI

                                                                       Mahrez
    Winga wa Leceister City aliye katika kiwango bora kwa sasa nchini England Mualgeria Riyad Mahrez amekiri kuwa huwa anafurahi sana watu wanapomfananisha na nyota wa FC Barcelona Muargentina Lionel Messi.

    Akifanya mahojiano na Telegraph,Mahrez,24 amesema "Watu wanapotaja jina langu na la Messi pamoja najisikia burudani sana kwasababu kwangu Messi ndiye nyota bora zaidi wa soka.Huwezi kumwambia kitu,yeye ndiye bosi.Naipenda pia FC Barcelona.Ninapokuwa nyumbani huwa sikosi kuitazama kila inapocheza.Alimaliza Mahrez ambaye mpaka sasa ameifungia Leceister City magoli 10 katika michezo 15 ya ligi kuu.

                                                                            Messi

    Akijibu swali juu ya lini atahama Leceister City,Mahrez amesema hana haraka ya kufanya hivyo na kusisitiza kuwa bado ana mapenzi makubwa sana na klabu hiyo inayosumbua vigogo England.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAHREZ ACHEKELEA KUFANANISHWA NA MESSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top