A. USAJILI
1. Kamati imepitisha usajili wa wachezaji walioombewa kwa vilabu vifuatavyo vya ligi
kuu
1. AZAM FC - mchezaji mmoja Ivo Philiph Mapunda (huru)
2. COASTAL UNION - wachezaji watatu
i. Omary Wayne Maunda-Mkopo toka Azam
ii. Miraji Adam Seleman-mkopo toka Simba
iii. Ramadhani Ali Thabit-huru
3. MGAMBO SHOOTING
i. Mudathir M. Khamis-Yanga
ii. Nurdin Mkomeni-huru
iii. Godson Mmasa-alikuwa mchezaji wa Mgambo, wameomba kumsajili tena
4. MTIBWA SUGAR
i. Alex Mwambisi-huru
ii. Boniface Maganga-Mkopo kutoka Simba
iii. Kelvin Iddi Friday-Mkopo kutoka Azam
iv. Abdallah Said Makangana-alisahaulika
usajili uliopita ni mchezaji anayendelea
5. MWADUI SC
i. Abdallah Mfuko-huru
ii. Ismail Gambo-Mkopo kutoka Azam FC
6. NDANDA SC
i. Braison Raphael-Mkopo kutoka Azam
ii. Jackson John Nkwera-Sinza Srtars
7. MBEYA CITY
i. Ramadhani Selemani Chombo-huru
ii. Abdallah Salum Juma-Toto Africans
iii. Deogratius Julius-Kagera Sugar
8. TANZANIA PRISONS
i. Baraka Majogoro-Wenda FC
9. TOTO AFRICANS
i. Shija Hassan Mkina-huru
ii. Frank B Kimati-huru
iii. Ladslaus Mbogo-huru
iv. Yusuf Seleman Mpili-huru
v. Maneno Steven Shaban-huru
10. SIMBA SC
i. Kiongera Raphael-Amerudishwa toka KCB
alikokuwa anacheza kwa mkopo
ii. Novaty Lufunga-African Sports
iii. Haji Mohamed Ugando-Jaki Academy
iv. Brian Majegwa-Azm FC
11. STAND UNITED
i. Assouman N’gueassan David-FC Olympic
Sports Abobo
12. YOUNG AFRICANS
i. Issoufou Boubacar-
ii. Paul Nonga-Mwadui
13. JKT RUVU
i. Waziri Shaban Iddi-huru
ii. Hamis Thabit-African Lyon
iii. Hassan Dilunga-Stand United
14. MAJIMAJI
i. Kennedy Stainley Kipepe-Njombe Mji
ii. Abubakar B Bakari-huru
iii. Sixmund Ally Mwakasekaga-huru
iv. Paulo Maona Terry-huru
15. KAGERA SUGAR
i. Ramadhani Mzee Kipalamoto-Kagera Sugar
ii. Samwel Donald Ngassa-huru
iii. Shaaban Ibrahim Sunza-Mshikamano
iv. Martin Lupart Mlolere-Abajalo, Dar es
Salaam
v. Juma Jabu Hamis-huru
16. AFRICAN SPORTS
i. Hamis Twairu Juma-U20, huru
ii. Hamad Nathaniel Mbumba-Polisi Tabora
iii. Hamad Nathaniel Mbumba-African Lyon
iv. Charles Martin Ilamfya-Mkopo toka Mtibwa
v. Rajab Isihaka-huru
vi. Reyna Mgungira-huru
USAJILI UFUATAO UMEZUILIWA KWA
MAELEZO YAFUATAYYO
1. AFRICAN SPORTS
i. Karim Hamud Juma aliyeombea kusajiliwa
na African Sports akitokea PolisiTabora usajili
wake
ii. Michael Victor Mgimwa kamati imezuia usajili wake mpaka hati ya uhamisho wa
kimataifa umezuiwa mpaka timu mbili zitakapofikia makubaliano itakapotumwa toka Thailand, mchezaji huyu alikuwa anaitumikia Rio United ya Thailand.
2. MAJIMAJI SPORTS CLUB
i. Danny David Mrwanda na Lulanga Andrew
Mapunda-kamati imezuia usajili wake mpaka
vilabu viwili vya Majimaji inayotaka kumsajili
na Lipuli iliyokuwa inawamiliki wachezaji hao
zitakapokubaliana na kutuma kwa maandishi
makubaliano yao TFF.
3. MBEYA CITY
i. Kamati baada ya uchunguzi imejiridhisha kwamba mchezaji Tumba Sued aliyewekewa pingamizi na Coastal Union alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na Coastal Union
siku ya tarehe 12 June, 2014 na mkataba huu ulienda kushuhudiwa kwa mwanasheria siku
ya tarehe 23 Agosti 2014, kushuhudiwa huku
hakukubatilisha mkataba uliosainiwa tarehe
12 June 2014.
Hivyo kamati inamtangaza Tumba Sued kuwa
mchezaji huru toka tarehe 11 Desemba na kwa
sasa ni mchezaji halali na amepitishwa
kuichezea Mbeya City ya Mbeya.
ii. Kamati pia inatoa onyo kali kwa klabu ya
Mbeya City na imeagiza kesi hii ipelekwe
kwenye kamati ya nidhamu kwa kuongea na
mchezaji Ditram Nchimbi ambaye ni mchezaji
halali wa Majimaji ya Songea ambaye alisaini
mkataba wa miaka miwili na Majimaji tarehe 20 Oktoba 2014 hivyo mkataba wake utaisha tarehe 19 Octoba 2016. Mbeya City wameongea na mchezaji mwenye mkataba uliozidi miezi 6 bila kuomba ridhaa ya klabu
inayommiliki ambayo ni Majimaji.
4. JKT RUVU
JKT Ruvu iliomba kumsajili mchezaji Hassan Dilunga kutoka Stand United kwa kufata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuongea na
klabu yake ya Stand United na kupata kibali cha kumsajili Dilunga kutoka kwa uongozi
halali wa Stand United kupitia kwa mwenyekiti na katibu wa Stand United. Pamoja na ruhusa kutoka kwa Stand United bado kuna mtu
anayeitwa mratibu wa Stand United aliiandikia barua TFF akipinga usajili wa mchezaji huyu.
Kamati imesikitishwa na kiendo cha mtu huyu
ambaye hatambuliki na TFF na wala siyo mtu anayepaswa kuwasiliana na TFF kwa kuingilia
maamuzi ya viongozi halali wa Stand United na imeamuru mtu huyo anayeitwa Mbasha Matutu apelekwe kamati ya maadili.
0 comments:
Post a Comment