Lubumbashi,DRC.
Ndoto ya Straika Mtanzania Mbwana Aly Samatta kucheza soka barani Ulaya inaelekea kutimia januari mwakani baada ya klabu yake ya TP Mazembe kukubali kumuuza kwenda klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayokipiga katika dimba la Cristal Arena.
Kwa mujibu wa L’Equipe ni kuwa mmiliki wa TP Mazembe Moïse Katumbi tayari ameshafikia makubaliano na KRC Genk juu ya ada ya Samatta na kilichobaki ni nyota huyo mwenye miaka 23 kusaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuichezea miamba inayoshika nafasi ya sita katika ligi ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler League.
MAFANIKIO
KRC Genk imetwaa mataji matatu ya ligi kuu Ubelgiji mwaka 1998–99 ,2001–
02 na 2010–11 .Pia imetwaa vikombe vinne ya kombe la ligi karibuni ikiwa ni 2008–09 na 2012–13 .
Pia KRC Genk imeweka historia ya kufuzu hatua ya makundi michuano ya Ulaya maarufu kama (UEFA Champions League) msimu wa 2002–03 na 2011–12.
NYOTA WALIOPITA KRC GENK
Yannick Ferreira Carrasco (Atlético Madrid), Jelle
Vossen (Club Brugge), Steven Defour ( RSC Anderlecht), Christian Benteke ( Liverpool
FC ), Thibaut Courtois Chelsea FC), Divock
Origi ( Liverpool FC) na Kevin De Bruyne ( Manchester City FC).
Dimba la Cristal Arena
0 comments:
Post a Comment