Munyonyo,Uganda.
Mshambuliaji aliye katika kiwango bora kwasasa nchini Uganda Farouk Miya juzi jumapili aliibuka kidedea baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo.
Miya aliyeiongoza Uganda Cranes kutwaa kombe la Chalenji nchini Ethiopia mwezi huu ametwaa tuzo hiyo inayojulikana kama Airtel-Fufa Player of the Year baada ya kuwashinda Kezironi Kizito anayecheza nae katika klabu ya Vipers na nyota wa Orlando Pirates Yasser Mugerwa.
Mbali ya tuzo hiyo pia Miya amezawadiwa gari dogo aina ya Toyota Premio kama zawadi ya kuwa mchezaji bora wa mwaka.
Nyota wengine waliotwaa tuzo mbalimbali ni:
Mchezaji bora kwa upande wa wanawake: Sandra Nabweteme
Tuzo ya Fufa Presidential : Paul Ssali
Kocha bora wa mwaka: Faridah Bulega
Mwamuzi bora wa mwaka: Mark Sonko
Tuzo ya Fufa Fairplay: SC Villa
Mpira wa ufukweni: Douglas Muganga
Mchezaji kipenzi cha mashabiki Uganda: Tony Mawejje
Mchezaji kipenzi cha mashabiki Afrika: Andre
Ayew (Ghana & Swansea)
0 comments:
Post a Comment