Leceister,England.
Kocha wa Leceister City Muitaliano Claudio Ranieri ambaye usiku wa jana aliiongoza klabu yake kurejea kileleni mwa ligi kuu nchini England baada ya kuilaza Chelsea kwa mabao 2-1 ametamba kuwa hakuna pesa itakayoweza kuwanunua nyota wake Jamie Vardy,28 na Riyad Mahrez,24.
Akijibu swali aliloulizwa baada ya mchezo wa jana kama atakuwa tayari kuwauza nyota hao ambao mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 26,Ranieri amesema katu hatarajii kuwaona nyota hao wakiondoka klabuni hapo mwezi januari ama katika majira ya kiangazi na amesisitiza kuwa hakuna pesa itakayoweza kuwanunua.
Kauli hiyo ya Ranieri imekuja baada ya hivi karibuni Vardy na Mahrez kuanza kuhusishwa na kutakiwa na vilabu vikubwa vya England kama Manchester United,Chelsea na Arsenal kufuatia kuendelea kuonyesha kiwango kikubwa cha kusakata kabumbu na kuiwezesha Leceister City kukaa kileleni mwa ligi kuu baada kufikisha pointi 35 katika michezo 16.
0 comments:
Post a Comment