London,England.
Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Muhispania Diego Costa anatarajia kuukosa mchezo wa siku ya jumatatu wa ligi kuu England utakaochezwa Old Trafford dhidi ya Manchester United baada ya kuwa na kadi tano za njano.
Costa,26 ambaye jana jumamosi aliifungia Chelsea mabao mawili katika mchezo uliokwisha kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Watford alilimwa kadi ya njano baada ya kuonyesha mchezo usio wa kiungwana na hivyo kufikisha kadi tano za njano ambazo humfanya mchezaji husika akose mchezo mmoja.
Kutokana na kukosekana kwa Costa katika mchezo wa jumatatu Chelsea italazimika kuwatumia Radamel Falcao ama Loic Remmy katika safu yake ya ushambuliaji
0 comments:
Post a Comment