Dortmund, Ujerumani.
Borussia Dortmund imetinga robo fainali ya michuano ya kombe la DFB Pokal baada ya kuitandika FC Augsburg kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa hatua ya 16 uliopigwa katika dimba la Augsburg Arena jana usiku.
Mabao yaliyopita ushindi Borussia Dortmund ambayo msimu uliopita ilipoteza mchezo wa fainali yamefungwa kipindi cha pili dakika za 61 na 72 na washambuliaji Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan.
Kufuatia ushindi huo Borussia Dortmund itavaana na VFB Stuttgart katika mchezo wa robo fainali utakaopigwa kati ya Februari 9 na 10 huku nusu fainali ikiwa April 19 na 20 na fainali ikichezwa Mei 21.
Michezo ya robo fainali itakuwa kama ifuatavyo..
VfB Stuttgart vs. Borussia Dortmund
VfL Bochum vs. Bayern München
Heidenheim vs. Hertha Berlin
Bayer Leverkusen vs. Werder Bremen
0 comments:
Post a Comment