Dar es salaam,Tanzania.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga leo jioni wameimalisha kikosi chao kwa kuwasajili Paul Nonga toka Mwadui FC na Issoufou Boubacar Garba "Diego" toka Niger.
Nonga aliyewahi kukipiga pia katika vilabu vya JKT Oljoro na Mbeya City amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa Yanga huku Garba yeye akipatiwa mkataba wa mwaka mmoja wenye uwezekano wa kurefushwa ikiwa ataonyesha maendeleo mazuri.
Kabla ya kutua Yanga Garba aliwahi kukipiga nchini Tunisia na vilabu vya Club Africain na ES Hammam-
Sousse.
0 comments:
Post a Comment