Haruna Niyonzima amekuwa akichelewa kurejea kikosini,
hii imekuwa ni dharau ya muda mrefu kwa viongozi na wanachama wa Yanga.
Sasa wamechoka!
Yanga imecharuka kuhusiana na Haruna Niyonzima kuonyesha dharau kwa uongozi na wanachama wa klabu hiyo Goal imegundua.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alikaririwa na Saleh Jembe amesema wamekuwa
hawafurahishwi kwa muda mrefu sasa kutokana na tabia za Niyonzima za
kuchelewa kujiunga na kikosi kila anapokwenda Rwanda.
“Niyonzima amekuwa na tabia ambayo si nzuri kwa maana ya nidhamu kila
anapokuwa kwao Rwanda. Mfano tumemruhusu kwenda kuitumikia Rwanda
katika michuano ya kimataifa, hadi sasa hajarejea.
“Angalia mchezaji wa Azam FC kama Mugiraneza ambaye anacheza timu
moja na Haruna amesharejea, wachezaji wa Simba waliocheza fainali wako
katika klabu yao.
“Niyonzima hajarejea na wala hasemi lolote. Si Jambo sahihi na hili
linaonyesha tabia isiyo sahihi kwa maana ya kuheshimu majukumu yake
katika klabu,” alisema Dk Tiboroha.
“Haruna amekuwa akifanya hivi mara kwa mara, lakini sasa tumechoka na
kama tutachukua hatua kali, basi wanachama wajue kabisa mapema.
“Tumekuwa tukitoa adhabu kwake mara kadhaa, lakini mambo
hayabadiliki. Wakati mwingine tumemkata mshahara hadi sasa tunaona kama
tumechoka, lakini mambo ni yaleyale.”
0 comments:
Post a Comment