Manchester, England.
Mlinzi wa zamani wa Liverpool na England Jamie Carragher ameishauri Manchester United kuhakikisha inamnasa kwanza kocha Pep Guardiola kabla haijafikiria kuwanasa Cristiano Ronaldo,Neymar Jr ama Gareth Bale.
Akifanya mahojiano na gazeti la Daily Mail Carragher ambaye pia ni mchambuzi wa soka katika luninga ya BT Sports amesema Manchester United inapaswa kuizidi kete Manchester City na kumchukua Guardiola kwani wachezaji wengi nyota duniani wanavutiwa kufanya kazi na kocha huyo ambaye mwishoni mwa msimu huu ataachana na Bayern Munich.
Carragher anaamini mbinu,mvuto,ushawishi na soka analofundisha Guardional ndiyo vitakavyoisaidia Manchester United kuwanasa Ronaldo na nyota wengine wenye majina makubwa duniani na siyo Louis Van Gaal ama aina ya soka linalochezwa na klabu hiyo kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment