Roma,Italia.
UONGOZI wa klabu ya AS Roma umemwambia kocha wake mkuu Rudi Garcia kuwa ahakikishe anashinda mchezo wa jumapili hii wa ligi ya Seria A dhidi ya Genoa vinginevyo atatimuliwa kibarua hicho mara moja.
Kauli hiyo kali imekuja kufuatia siku ya jumatano AS Roma kutupwa nje ya michuano ya Coppa Italia baada ya kukubali kichapo cha penati 4-2 toka kwa klabu ya Seria B ya Spezia.
Taarifa kutoka Sky Sport Italia zinasema kuwa baada ya kichapo hicho kocha Rui Garcia aliwekwa kitimoto na wakurugenzi wa klabu hiyo na kutakiwa abadili hali ya mambo klabuni kabla maamuzi magumu dhidi yake hayajafikiwa.Kwani hivi karibuni AS Roma " Giallorossi" imeshindwa kupata ushindi wowote tangu Novemba 8 ilipoifunga SS Lazio katika mchezo wa Seria A huku pia ikishindwa kufunga bao hata moja katika michezo yake mitatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment