Southampton, England.
Arsenal imeshindwa kukalia kiti cha uongozi wa ligi kuu England baada ya usiku wa leo kukubali kichapo cha goli 4-0 toka kwa Southampton katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa St.Mary,Southampton.
Magoli ya Southampton yamepatikana dakika za 19,55,69,na 90 kupitia kwa Cuco Martina,Shane Long aliyefunga mara mbili na Jose Rui Fonte.
Kufuatia kichapo hicho Arsenal imebaki katika nafasi yake ya pili ikiwa na pointi zake 36 pointi mbili chini ya Leceister City yenye pointi 38 nafasi ya tatu inashikiriwa na Manchester City yenye pointi 35.
0 comments:
Post a Comment