Ibadan,Nigeria.
CHAMA cha waamuzi wa soka nchini Nigeria (NRFA) kimepata pigo baada ya mwamuzi wake Basil Giwa kufariki dunia jana jumatano wakati akifanyiwa mazoezi ya utimamu wa mwili maarufu kama (Cooper Test) kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa katika eneo la tukio huko kaskazini mashariki mwa mji wa Ibadan ni kuwa Giwa alidondoka na kupoteza maisha wakati akiendelea na mazoezi ya kuweka mwili sawa ambayo hufanyika ili kubaini utimamu wa miiili ya waamuzi kabla ya kupewa majukumu.
Mpaka tunakwenda mitamboni chanzo hasa cha kifo cha Giwa kilikuwa bado hakijafahamika.
0 comments:
Post a Comment