London,England.
Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amemtaja N’Golo
Kante wa Leicester City kuwa ndiye usajili bora zaidi wa mwaka 2015 ligi kuu nchini England kuliko Dimitri Payet wa West Ham United na Petr Cech wa Arsenal.
Carragher ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha BT Sports amesema Kante,24 aliyejiunga na Leicester City msimu huu akitokea Stade Malherbe
Caen ya Ufaransa amefanya kazi nzuri sana na kuwa mchango mkubwa kwa klabu hiyo ya King Power iliyoko kileleni mwa ligi kuu nchini England.
Mpaka sasa Kante ameifungia Leceister City bao 1 na kutengeneza nafasi 16 za kufunga katika michezo 17 ya ligi kuu akiwa na usahihi wa pasi wa 82%,usahihi wa mashuti wa 33%,amecheza mipira 14 ya kichwa,kukokota mpira mara 13 na amefanya tackling 49
Aidha Carragher amekiri kuwa kama kiungo wa Westham Dimitri Payet asingepata majeruhi na kukaa nje ya uwanja basi huenda angefanya vizuri kuliko Mfaransa mwenzie N’Golo
Kante.
0 comments:
Post a Comment